2013-03-02 10:21:17

AMECEA ni kati ya watazamaji wa uchaguzi mkuu nchini Kenya


Tume ya haki na amani ya Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya imeialika Tume ya Haki na Amani ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati, AMECEA kuwa ni kati ya watazamaji katika mchakato wa uchaguzi mkuu nchini Kenya unaotarajiwa kufanyika Jumatatu, tarehe 4 Machi 2013.

Wananchi wa Kenya Millioni 14 wanatarajiwa kushiriki katika zoezi hili muhimu kama kipimo cha ukomavu wa demokrasia inayotafuta mafao ya wengi sanjari na kujenga umoja na mshikamano wa wananchi wa Kenya. Timu ya AMECEA itawashirikisha pia wasomi kutoka Chuo Kikuu cha Kikatoliki Afrika Mashariki na Kati, CUEA. Kwa mara ya kwanza wananchi wa Kenya wanapiga kura kwa kutumia Katiba Mpya iliyopitishwa kunako mwaka 2010.







All the contents on this site are copyrighted ©.