2013-03-01 07:30:36

Vuteni subira! Yesu bado anatenda miujiza ndani ya Kanisa lake!


Bila shaka waamini wengi wanalikumbuka lile tukio la Yesu kuwatetea wafuasi wake waliokuwa wamekaa siku nzima wakimsikiliza kwa makini, alipoambiwa na Mitume kwamba, kulikuwa kunakuchwa awape ruhusa watu waende kujitafutia chakula vijijini kwani pale palikuwa ni uwanda na nyika tupu!

Padre Francesco Rossi de Gasper mtaalam wa Maandiko Matakatifu anasema, Ukristo unaweza kufahamika kihistoria, lakini unamwelekeo katika maisha ya milele kwani unapita ufahamu na mwelekeo wa kihistoria. Ni dini ambayo inajikita katika eneo la kijiografia na muda; mambo yote haya ni muhimu sana katika kutangaza Hbari Njema ya Wokovu, ili iweze kupenya katika mioyo na maisha ya watu wengi zaidi; kwa kutoa kipaumbele cha kwanza na kuheshimu utu wa mwanadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu.

Jangwa linaweza kuelezwa kuwa ni kielelezo cha uwepo wa dhambi inayoharibu bustani nzuri iliyotengenezwa na Mwenyezi Mungu katika maisha ya mwanadamu. Yesu akawaambia wanafunzi wake si lazima waende, wapeni ninyi chakula! Yesu akafanya muujiza kwa kuwalisha watu elfu tano, bila kuhesabu wanawake na watoto. Yesu bado anatenda miujiza kwa ajili ya Kanisa lake! Vuteni subira!








All the contents on this site are copyrighted ©.