2013-03-01 12:01:56

Roma yaanza kusali kwa ajili ya mchakato wa kumpata Papa Mpya!


Kardinali Agostino Vallini, Makamu Askofu Jimbo kuu la Roma, kwa niaba ya Waamini wa Jimbo la Roma, anapenda kumshukuru Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, ambaye ameng'atuka rasmi kutoka madarakani kwa kumhakikishia kwamba, wataendelea kusali kwa ajili yake na Kanisa, wakati huu Makardinali wanapoanza mchakato wa uchaguzi wa Papa Mpya, ili kuendeleza dhamana na utume wa Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Kardinali Vallini anawaalika viongozi wa Kanisa kutumia fursa hii pia kutoa Katekesi ya kina kuhusu Ukulu na Dhamana ya Mtakatifu Petro katika kuliongoza Kanisa la Kristo, pamoja na kusali kwa ajili ya kumpata Papa Mpya. Anaendelea kuwaalika Watawa wa Mashirika ya ndani kusali zaidi kwa ajili ya mchakato wa kumpata Khalifa Mpya wa Mtakatifu Petro.







All the contents on this site are copyrighted ©.