2013-03-01 15:29:07

Makardinali kuanza mchakato wa kumtafuta Papa Mpya hapo tarehe 4 Machi 2013


Kardinali Angelo Sodano Dekano wa Makardinali katika taarifa yake kwa vyombo vya habari anasema kwamba, mkutano wa kwanza wa Makardinali watakaoshiriki katika mchakato wa kumchagua Papa Mpya utaanza rasmi, Jumatatu, tarehe 4 Machi 2013, saa 3:30 katika Ukumbi wa Sinodi ya Maaskofu. Kuna uwezekano pia wa kufanyika mkutano wa pili baadaye jioni.







All the contents on this site are copyrighted ©.