2013-02-28 11:28:04

Makardinali wanamshukuru Baba Mtakatifu Benedikto XVI


Kardinali Angelo Sodano, Dekano wa Makardinali kwa niaba ya Makardinali wote, Alhamisi, tarehe 28 Februari 2013 amemshukuru na kumpongeza Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita kwa ushuhuda wa huduma za kitume, kwa ajili ya mafao ya Kanisa na ulimwengu kwa ujumla.

Anamshukuru Baba Mtakatifu kwa maneno na wosia aliowaachia mara baada ya kuhitimisha mafungo ya kiroho, pale alipowaambia kwamba, wametekeleza wajibu wao kwa weledi, upendo na imani thabiti katika kumsaidia kutekeleza utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Makardinali wanamshukuru kwa ushuhuda wa maisha na utume katika kipindi chote cha miaka minane ya uongozi wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro. Lakini, kwa namna ya pekee, wakati huu anapong'atuka kutoka madarakani, ili kutoa nafasi kwa Kiongozi mwingine, kuliendeleza Kanisa. Kuna mengi ambayo wamejifunza kutoka kwake kama walivyokuwa wale wafuasi wa Emmaus walipokuwa wanatembea na Kristo wakibadilishana mawazo kuhusu tukio kubwa katika maisha yao!







All the contents on this site are copyrighted ©.