Jopo la Makardinali lililochunguza uvujaji wa nyaraka za siri kutoka Vatican lakutana
na Papa Benedikto XVI
Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, Jumatatu, tarehe 25 Februari 2013 amekutana
na Jopo la Tume ya Makardinali watatu: Julian Herranz, Joseph Tomko na Salvatore de
Giorgi waliokuwa wamepewa dhamana ya kuchunguza uvujaji wa nyaraka za siri kutoka
Vatican. Jopo hili liliongozana pia na Padre Luigi Martignani, O.F.M.
Baada
ya kuhitimisha kazi yao, Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, amewashukuru Makardinali
hawa kwa kazi kubwa waliyoifanya. Uchunguzi wao umedhihirisha udhaifu wa binadamu
unaoweza kujitokeza katika taasisi yoyote ile, bila kusahau kwamba, kuna watu wengi
zaidi wanaotekeleza wajibu na dhamana yao kwa ukarimu, unyofu na sadaka kubwa, kwa
ajili ya huduma kwa Kanisa na kwa Khalifa wa Mtakatifu Petro.
Baba Mtakatifu
Benedikto wa kumi na sita ameamua kwamba, taarifa ya uchunguzi iliyofanywa na Jopo
la Tume ya Makardinali itatolewa kwa Papa Mpya peke yake!