2013-02-25 09:17:23

@pontifex kusitishwa hadi Papa mpya atakapochaguliwa!


Monsinyo Paul Tighe, katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano ya Jamii anabainisha kwamba, tangu pale Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, atakapong'atuka rasmi kutoka madarakani, tarehe 28 Februari 2013, saa 2:00 Usiku, akaunti yake ya twittwer, itasitishwa hadi pale Makardinali watakapokuwa wamekamilisha mchakato wa uchaguzi wa Papa Mpya ambaye ataamua nini cha kufanya! Hadi sasa kuna takribani wafuasi millioni tatu ambao wamejiunga kwenye Akaunti ya Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita.







All the contents on this site are copyrighted ©.