2013-02-23 16:32:24

Barua ya Kitume ya Papa kwa Kardinali Gianfranco Ravasi.


Baba Mtakatifu Benedikto XV1, Jumamosi mchana amekamilisha wiki la mazoezi na tafakari za kiroho kwa ajili ya kipindi cha kwaresima. Mafungo yaliyoongozwa na Kardinali Gianfranco Ravasi, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya utamaduni.
Akimalisha mafungo haya, alitoa barua yake ya kitume kwa Kardinali Gianfranco Ravasi, ambamo amemshukuru kwa moyo wa dhati kwa sadaka ya kuwaongoza kiroho katika kipindi hiki muhimu cha ukimya, mafungo na mazoezi ya kiroho ya wakati wa kwaresima kwa Yeye Papa na wasaidizi wake na wafanyakazi katika idara za Curia ya Roma.
Papa ameutaja muda wa ukimya na mazoezi ya kiroho na sala kuwa ni vyema na muhimu, maana umewazesha kuitafakari kwa kina Mada ya mwaka huu, "Mazugumzano kati ya Mungu na binadamu katika sala ya Mzaburi".
Barua ya Papa imekiri kwamba, muda huu umekuwa ni msaada mkubwa, hasa katika kujifunua kiroho, na kuzungumzia ukame wa kiroho katika nyayo za Yesu jangwani,na hivyo wameweza kupata nguvu za kufika katika chemichemi ya maji safi na mengi ya Neno la Mungu, na kuteka neema nyingi kutoka Kitabu cha Zaburi, na Maandiko mengine ya Biblia, ambayo hutengeneza sala ya muumini.
Na katika utajiri wa utambuzi na uzoefu wake wa kitaaluma, ameweza kuionyesha safari ya kuvutia kwa njia ya sala ya Zaburi, katika uchaguzi wa kupanda na kushuka.
Papa ametaja sala za Zaburi kwamba, katika ukweli hulenga hasa kuelekea uso wa Mungu kwa fumbo katika akili ya binadamu ambaye mwovu, lakini Neno hili la Mungu, kwa mara nyingine humruhusu binadamu kuona tena Mungu akijifunua kwetu. Na ni katika wakati huo huo, mwanga huo, huangaza kutoka uso wa Mungu, na sala ya Mzaburi, hutuongoza katika kuutazama uso wa mtu, katika utambuzi wa ukweli wa furaha yake na huzuni, wasiwasi na matumain yake.

Maelezo ya Papa , yanasema Yeye mwenyewe kama Khalifa wa Petro na wassaidizi wake, wameitwa kutoa kwa Kanisa na ulimwengu, kuishuhudia waziwazi imani ya Kanisa , na hili linawezekana tu kupitia moyo wa shukurani, uliozamishwa katika kina cha ukimya na katika kuzungumza na Mungu, hasa kwa ajili ya kutoa jibu kwa swali linalo ulizwa na watu wengi," Upi i upendo wa Mungu?Jibu la haraka kwa swali linatolewa na Mzaburi, Bwana amenitia furaha moyoni mwangu kupitia wao wanapozidishiwa nafaka na divai. taz. Zab 04:07).

Na mwisho Papa alitoa shukurani zake kwa wote si kwa ajili ya kushiriki tu katika wiki la mazoezi ya kiroho lakini pia kwa kufanya kazi nae kwa kipindi cha miaka minane, katika lengo hili la kulifikisha neno na upendo wa Mungu kwa watu wote kupitia utume wa Petro. Na amewahakikishia kwamba , kuptia sala , daima atakuwa karibu nao. Na pia ndani mwake kumebaki shukurani hizi, hata kama sasa anajiuzuru katika kiti cha Petro , bado yuno katika usharika kanisa na sala. Na kwa namna hiyo kuna uhakika wa Kanisa kusonga mbele na ushindi wa uhakika na ukweli wa uzuri na Upendo wa Mungu.








All the contents on this site are copyrighted ©.