Imani na sayansi katika utetezi wa Maisha ya binadamu
Katika kilele cha Mkutano Mkuu wa 19 juu ya Imani na Maisha ya Binadamu wa Taasisi
ya Kipapa kwa ajili ya Elimu ya Maisha, mkutano wa siku tatu, kwa mwaka huu umeongozwa
na Mada : Imani na Maisha ya binadamu katika sayansi.
Katibu Mratibu wa Taasisi
hiyo, Padre Scott Borgman, akizungumza na Redio Vatican , alieleza kwamba, Taasisi
hiyo , ni nafasi ya kufanya gunduzi na tafakari makini juu ya thamani ya maisha ya
binadamu katika dunia ya leo. Na ni chombo si tu kwa manufaa ya Vatican lakini kwa
kanisa lote la ulimwengu, na dunia kwa ujumla.
Katika maelezo yake, kwanza
kabisa alikanusha dhania kwamba taasisi hiyo imejaa Mapadre na maofisa wa Vatican.
Bali ni chombo cha wanasayansi na wasomi watalaam ambao hujikita katika kuchambua
hoja zinazowaka moto leo hii, kama vile haki ya maisha, jenda, na utetezi wa maisha
na familia , katika kutaja machache.
Na kwamba, katika mikutano yao kuna mapadre
au makreli wachache, na hivyo wengi wao ni walei wanaofanyakazi katika hospitali mbalimbali
na taasisi nyingine za kisayansi duniani. Kwa mkutano huu wa Roma ulikamilika ulihudhuriwa
na wajumbe 120, walio shiriki kuichambua mada ya Mkutano ya mwaka huu: Imani na maisha
ya binadamu. Katika mada hii, washiriki wa Mkutano wamelenga zadi katika Kanisa
na Maandiko Matakatifu, yanavyo tufundisha juu ya asili ya maisha ndani ya familia
iliyosimikwa katika misingi ya maisha ya ndoa kati ya mwanamme na mwanamke. Askofu
Mkuu Muller, Mkuu wa Shirika la Mafundisho Sadikifu, amezungumzia juu ya maisha ya
binadamu kwa mujibu wa mafundisho ya Kanisa na msingi wa utendaji wote wa kibiolojia
na tiba , katika kuheshimu maisha ya kila biandamu na pia asili ya maisha ya binadamu
katika ndoa ya mke na mme na familia. Mwaka jana, kati ya mengine mkutano ulizungumzia
tatizo la ugumba , na matumizi ya kondo la binadamu katika maabara.