2013-02-22 10:56:54

Dr. Jacob Chilemedya achaguliwa kuwa Askofu mkuu wa Kanisa Anglikani, Tanzania


Kanisa Anglikani Tanzania limemchagua Askofu Jacob Chilemedya kuwa Askofu mkuu wa Kanisa Anglikani Tanzania. Huyu anakuwa ni Askofu wa sita kushika wadhifa huu baada ya Askofu mkuu Valentino Mokiwa kumaliza muda wake kwa mujibu wa Katiba ya Kanisa Anglikani.

Askofu mkuu mteule Chilemedya alizaliwa kunako Mwaka 1957. Alipata shahada ya kwanza kutoka katika Chuo cha Mtakatifu Philipo, kilichoko Mkoani Dodoma. Baadaye aliendelea na masomo yake nchini Kenya kwenye Chuo cha Mtakatifu Paulo na hatimaye, kupata shahada ya uzamili kunako mwaka 2003 kutoka Marekani. Mwaka 2007 Dr. Chilemedya aliteuliwa kuwa Askofu mwandamizi wa Jimbo la Mpwapwa chini ya Askofu Simoni Chiwanga na baadaye akateuliwa kuwa Askofu wa Dayosisi ya Mpwapwa, Kanisa Anglikani.

Askofu mkuu mteule Chimeledya anatarajiwa kuwekwa wakfu mwishoni mwa Mwezi Mei, 2013 mjini Dodoma.







All the contents on this site are copyrighted ©.