2013-02-22 16:04:42

Benedikto XV1, ni mfano wa maisha ya imani hata kwa Waluteri


Mchungaji Jens Martin Kruse, wa Jumuiya ya Kiinjili ya Kiluteri hapa Roma, akii tafakari miaka minane ya utawala wa Papa Benedikto XV1, amemtaja kuwa mfano mzuri wa kuigwa na waamini si Wakatoliki tu lakini hata Waluteri.

Anasema, tangu siku ya kwanza ya kuchaguliwa kwake,hapo 19 April 2005, Papa Benedikto XV1, alitangaza katika ujumbe wakekwa kwanza kwa Makardinali kwamba, uekumene itakuwa kati ya kipaumbele katika utawala wake na hivyo alionyesha toka mwanzo kwamba ataelekeza nguvu za kazi zake, na bila ya kujibaki katika ujenzi wa umoja kamili wa kuonekana wa Wafuasi wote wa Kristu.

Mchungaji Jens anaendelea na maelezo yake kwamba, hivyo kujiuzuru kwa Papa kunaendelea kutoa ufahamu zaidi kwamba, kwake yeye, kuyatimiza mapenzi ya Bwana, na kuiishi imani, si tu kung’ang’ana na mamlaka au mimbali, lakini ni kupitia uthabiti wa imani inayotoka ndani yamtima wa moyo, na kuingia katika dhamiri na kutoa msukumo unaoonyesha kwa kila mtu kwamba, ndani uongofu mna mwendelezo wa utendaji na utendaji wote wa kiekumeni.

Anasema, wote waliofanya kazi kwa karibu na utawala wa Papa Benedict XVI, wameweza kuionja hamu hii ya Benedikto XV1, katika kujenga uekumeni na umoja wa kweli wa Wakristu. Kuna ishara nyingi zinazo onyesha hamu hiyo, ya kuiendeleza safari ya kuelekea umoja kamili kwa wafuasi wa Kristu.

Mchungaji Jens ametaja machache yanayothibitisha nia hiyo ya Papa Benedikto xv1, kuwa ni pamoja ziara yake ya 14 Machi 2010 alipotembeela Jumuiya ya Kiinjili la Kilutheri katika kanisa la Kristu Mfalme. Kwao ilikuwai ni ishara ya pekee sana ya dhamana ya kiekumeni. Wengi walijiuliza kwa jinsi Papa kama kiongozi wa Kanisa Katoliki, alivyo weza kuwa na nguvu za kujumuika katika sherehe ya Waluteri wa hapa Roma, ambamo alishiriki ibada katika utamaduni wa Kilutheri. Hilo lilionyesha kwamba kweli Papa anayo nia ya kujenga uekumeni wa kweli.
Tukio jingine liilowavutia Waluteri ni Papa alipotembelea jengo lililokuwa la watawa Wa Mtakatifu Agostine, la Erfurt Ujerumani, hapo Septemba 23 , 2011. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Papa kuingia katika jengo hilo ambako Martini Luter alipewa daraja la Upadre na kusoma Ibada ya Misa kwa mara ya kwanza. Mahali hapo, Papa na Maaskofu Waluteri wa Ujerumani walikusanyika katika Ibada iliyosomwa katika mapokeo ya Kiluteri. Katika hotuba yake Papa alitoa shukrani zake kwa uwezekano huo wa Wakaristu kuketi pamoja mahali hapo. Na hivyo ziara hii ya Papa Benedikto XV1, Erfurt, ni kitendo cha hali ya juu kinachonyesha moyo wa ushariki na Umoja katika Kristu .
Pamojana utendaji mwingine mwingi, Papa amekuwa ni mfano wa jinsi Wakristu licha ya kuwa na mtazamo mbalimbali kiliturujia, bado wanaweza kukutana pamoja na kumshuhudia Kristu, kuwa ndiye mkombozi pekee wa duniani. Na binadamu ni mhujaji katika njia inayoongozwa na Mungu.









All the contents on this site are copyrighted ©.