2013-02-21 15:54:48

Wakati wa Utupu katika Kiti cha Khalfa wa Mtume Petro..


Masharti ya Kanuni ya Sheria ya Kanisa juu ya Dekania ya Makardinali.
Makardinali ni washauri wa ngazi ya juu wa karibu sana wa khalifa wa Mtume Petro, katika utendaji wote wa kanisa la Ulimwengu. Na kuteuliwa kwao na Papa , hutangazwa rasmi katika Mkutano wa Makadinali unaojulikana kwa jina Consistory.
Historia inaonyesha mwaka 1958, Papa John XXIII, aliweka miaka 70, kuwa ukomo wa umri wa Kardinali kuwa na haki ya kupiga kura ya kumchagua Papa mpya. Na pia alipitia sheria ya Makadinali wote kupewe hadhi ya Kiaskofu. Lakini mwaka 1970, Papa Paulo VI aliongeza ukomo wa umri wa Kardinali kukosa haki ya kupiga kura ya kumchagua Papa kuwa miaka 80.
Na kulingana na sheria ya Kanisa namba 349, utendaji wa dekania ya Makadinali, umetengwa katika vipengere vitatu msingi kusimamia :
Ni kumchagua Khalifa wa Kiticha Petro, Papa au Baba Mtakatifu, ambaye pia huwa Askofu wa Jimbo la Roma;
Kutoa ushauri kwa Askofu wa Roma , katika mkutano wa Makadinali Consistory, juu masuala ya muhimu kwa Kanisa la Ulimwengu.
Na Kardinali kama watu binafsi, kutoa msaada wake kwa Baba Mtakatifu na Askofu wa Roma, katika huduma za kila siku za Kanisa zima la ulimwengu, na ofisi za idara ya Curia ya Roma, na Rais wa Sekretarieti ya Nchi, kwa Wakuu wa Idara za Curia ya Roma na Manaibu wa Kitume Ofisi za Utiaji wa Sahihi ya Kipapa, na wajumbe wa Bodi na Rais wa Idara kwa ajili ya masuala ya kiuchumi, na Rais wa Mahakama ya Kitume ya Kitubio, pamoja na utawala katika mambo ya Mali za Makao Makuu ya Kitume, kama ilivyo elezwa katika sheria za kanisa namba 358 na 360.








All the contents on this site are copyrighted ©.