Tamko kuhusu mabadiliko katika Conclave-- Pd. Lombardi
Katika mkutano wa wanahabari wa mapema siku ya Jumatano, Mkurugenzi wa Ofisi ya Uchapishaji
ya Vatican na msemaji wa Papa , Padre Federico Lombardi, alieleza kwamba, Papa Benedikto
XV1, anafikiri kuchapisha tamko lake binafsi(Motu Prioprio) hivi karibuni , kwa nia
ya kutoa ufafanuzi katika vipengere kadhaa vya sheria zinazo tawala wakati Kiti cha
Petro kitakapo kuwa wazi na pia juu kikao cha Makardinali cha kuchagua Papa Mpya
(Conclave). Na kwamba ufafanuzi huo, kama ataufanya itakuwa kabla ya kujiuzuru
kwake rasmi hapo tarehe 28 Februari.
Padre Federico Lombardi anafikiri hati
hiyo ya Papa Benedikto,pengine itatoa ufafanuzi juu ya vipegere kadhaa kwa ajili ya
kuainisha sheria kadhaa zinazotumika wakati Kiti cha Petro kinapokuwa wazi na pia
Conclave. Na kwamba , uainishaji huo unategemea maamuzi yake Papa, vinginevyo kwa
wakati huu sheria zote zinabaki kama zilivyo.
Hivyo mpaka sasa, Kardinali
Tarcisio Bertone, Katibu wa Vatican, aliyeteuliwa kuwa Camerlengo hapo April 4, 2007,
ndiye atakuwa Msimamizi mkuu wa jimbo la Papa na Kanisa la Ulimwengu, wakati wote
Kiti cha Petro kitakapobaki wazi, baada ya Papa Benedikto XV1, kujiuzuru rasmi, saa
mbili za usiku, tarehe 28 Februari, 2013, hadi hapo Khalifa mwingine atakapochaguliwa. Pia
kwa cheo hicho, Kardinali Tarcisio anakuwa ni kiongozi Mkuu wa Mahakama ya Kitume
na sahihi ya Kitume, pia Mtunzaji na msimamizi mkuu wa mali na haki za Jimbo Takatifu
katika muda huo wa utupu. Katika kipindi hiki, kwa mujibu wa sheria ya "Universi
Dominici Gregis", wanaohusika na utendaji wa kazi za jimbo la Papa katika ngazi mbalimbali
hata walioteuliwa na Papa, hawapotezi nafasi zao , bali wanaendelea na majukumu yao
kama kawaida, chini ya Decania ya Makardinali, kama walivyokuwa wakiwajibika kwa Baba
Mtakatifu Mwenyewe.
Katiba hiyo inaeleza, mihuri na yaliyomo katika chumba
Papa,licha ya chumba cha Papa kufungwa rasmi, wafanyakazi wa kawaida wanaohudumia
katika makao binafsi ya Papa, wanaweza kukaa mpaka hadi hapo baada ya mazishi, au
kuteuliwa kwa Papa Mpya.
Usimamizi wote kazi na uwajibikaji, katika kipindi
cha Kiti cha Petro kuwa wazi, unaogozwa na Camerlengo akisaidiana na Makardinali wengine
watatu, hasa katika utatauzi wa masuala madogomadogo lakini muhimu , kama ilivyoelezwa
katika sheria za kanisa ( Ibara ya 7).
Jopo hilo la Camerlengo na wasaidizi
wake Makardinali watatu, wanayo mamlaka ya kuamua lini waanze Mkutano wa dekania
ya Makardinali kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi wa Papa, kwa mujibu wa Ibara namba
11.
Ni wajibu wa Camerlengo na pamoja na wasaidizi wake watatu Makardinali
kusimamia utendaji wote wa wakati huo na kutunza siri zote za wakati wa upigaji kura
katika mkutano wa conclave, unaofanyika katika kikanisa cha Sistine,cha ndani ya jengo
la Kipapa la Vatican. Na pia camerlengo ndiye anahusika na hatua ya kuchoma makaa
yenye kutoa moshi mweupe na kumtagaza Papa mpya alyechaguliwa na Makardinali katika
kikao hicho cha Conclave.