2013-02-21 14:04:42

Papa kukutana na Makardinali watakaokuwepo Roma, 28 Februari 2013


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, hapo tarehe 28 Februari 2013, kuanzia saa 5:00 asubuhi, atafanya mazungumzo ya faragha na kila Kardinali atakayekuwepo mjini Roma kwa wakati huo na baadaye atakutana na Makardinali wote kwa pamoja.

Hii itakuwa ni mara ya mwisho kwa Dekania ya Makardinali kuweza kuzungumza ana kwa ana na Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita kama Khalifa wa Mtakatifu Petro.







All the contents on this site are copyrighted ©.