Kardinali Gianfranco Ravasi, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Utamaduni, katika
siku ya tatu ya tafakari na mafungo ya Kiroho kwa Wakazi wa jengo la Kipapa na wafanyakazi
wa Curia ya Roma, alitazama zaidi matukio ya kanisa ya kihistoria na maelezo ya juu
ya Masiya katika Zaburi. Kardinali Ravasi , ameitaja historia kuwa ni mahali
pa kukutana na Mungu. Historia inatuonyesha jinsi tunavyoweza kukutana na Mungu kupitia
matukio mbalimbali kwenye hali zote , uchungu na mateso katika maisha na furaha
pia, kama ilivyojionyesha katika historia ya mwana wa Mungu, aliyemwilishwa na kuja
kukaa kwetu. Katika kuyatafakari maisha ya mtu, historia yake daima, inakuwua
ni nafasi inayo faa kukutana na Bwana Mungu wetu. Inaweza ikawa kupitia kashfa au
madhulumu, hata katika nchi ambamo kwa mara nyingi tunauona ukimya wa Mungu, na pia
katika mataifa ambako ukana Mungu umeshamiri. Aliendelea kufafanua kwamba, hata
katika kiini cha mema yote, tunapaswa kupata utambuzi kwamba , historia si tu mfulululizo
wa matukio yasiyokuwa na maana,hata katika utendaji wetu mdogomdogo, na pengine
katika majaribu na masumbufu, kama tunavyosoma katika kitabu cha Ayabu, yote hufanyika
kwa mapenzi ya Mungu. Na kwa namna hiyo, binadamu huweza kuiimarisha imani yake na
kusadiki zaidi kwamba, yupo mwenye uweza zaidi, anayetusindikiza katika hija yetu
hapa duniani. Ni Yeye Mchungaji anayetulinda dhidi ya kila asili na historia za hatari,
anayeandamana nasi katika safari ya kuelekea katika uhuru kamili. Na kwamba, tunapaswa
kuishi kwa tumaini, tumaini lisiolobadilika . Mungu wetu kama ilivyoelezwa katika
Kitabu cha Kutoka sura ya tatu , Ni mungu asiyekuwa na Jina , ni Mimi niko na ambaye
niko, kama alivyomwambia Musa, ndivyo utakavyo waambia wana wa Israel , "Mimi niko",
ndiye aliyenituma. Na hivyo kumbe , binadamu anayeiishi na kulikubali neno hili anajenga
mahusiano yake na Yeye aliyeko , katika uaminifu wake na katika mazungumzano nae na
katika kukutana na kuishi pamoja.