2013-02-19 11:44:20

Biashara ya silaha duniani kwa mara ya kwanza inaonja makali ya myumbo wa uchumi kimataifa!


Taarifa ya kituo cha utafiti cha kimataifa kijulikanacho kama "Stockholm International Peace Research Institute, SIPRI" kinabainisha kwamba, kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka kumi, biashara ya silaha kimataifa imeshuka kutokana na athari za myumbo wa uchumi kimataifa. Wateja wa kuu wa soko la silaha duniani ni Amerika na Ulaya Mashariki.

Kuna baadhi ya Makapuni yanayotengeneza silaha yamepunguza shughuli zake za uzalishaji na baadhi ya Makampuni yamejikuta yakifunga uzalishaji kutokana na hali ngumu ya uchumi kimataifa. Katika kipindi cha Mwaka 2011 pato la biashara ya silaha duniani lilikuwa ni kiasi cha dolla za kimarekani billioni 410, pungufu ya asilimia tano, ikilinganishwa na pato la Mwaka 2010.

Fedha hii ni sawa na Pato Ghafi la Taifa la Venezuela au Uswiss. Mabadiliko ya teknolojia katika masuala ya ulinzi na usalama yanaendelea kuathiri uzliashji wa silaha, ingawa bado kuna wasi wasi wa vitendo vya kigaidi kutokea sehemu mbali mbali za dunia. Utafiti uliofanywa na SIPRI ulishindwa kupata takwimu na taarifa kutoka China.

Wachunguzi wa mambo wanasema, bado biashara ya silaha ndogo ndogo inaendelea kushika kasi. Marekani inaongoza, ikifuatiwa na Ufaransa, Japan, Ujerumani, Brazil na Italia.







All the contents on this site are copyrighted ©.