2013-02-16 07:37:01

Rais Traian Basescu akutana na Papa Benedikto XVI mjini Vatican


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, Ijumaa, tarehe 15 Februari 2013 amekutana na kuzungumza na Rais Traian Basescu wa Romania ambaye pia alikutana na viongozi waandamizi kutoka Vatican chini ya Kardinali Tarcisio Bertone, Katibu mkuu wa Vatican.

Viongozi hawa wawili wamefanya mazungumzo yao katika hali ya kirafiki kwa kuangalia uhusiano kati ya Vatican na Romania, lakini zaidi uhusiano huu katika ngazi ya Bara la Ulaya, kama sehemu ya mchakato unaopania kulinda na kudumisha tunu msingi za maisha ya binadamu. Wamegusia pia mafanikio na matarajio ya ushirikiano kati ya Kanisa Katoliki na Serikali ya Romania katika sekta ya elimu.

Rais Basescu kwa niaba ya wananchi wa Romania amemshukuru Baba Mtakatifu kwa mchango wake kwa Kanisa Katoliki kama Khalifa wa Mtakatifu Petro. Amekuwa ni msaada mkubwa kwa maendeleo ya Waamini wa Kanisa Katoliki kutoka ndani na nje ya Romania.







All the contents on this site are copyrighted ©.