2013-02-16 12:02:14

Askofu mkuu Aldo Cavalli ateuliwa kuwa Balozo wa Vatican nchini Malta


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, amemteua Askofu mkuu Aldo Cavalli, kuwa Balozi Mpya wa Vatican nchini Malta, kabla ya uteuzi huu, Askofu Mkuu Cavalli alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Colombia. Askofu mkuu Cavalli alizaliwa kunako tarehe 18 Oktoba 1946 nchini Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapadrishwa kunako tarehe 18 Machi 1971.

Aliteuliwa na Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili kuwa Askofu mkuu na Balozi wa Vatican nchini Sao Tome na Principe, hapo tarehe 2 Julai 1996. Akawekwa wakfu kunako tarehe 26 Agosti 1996. Kunako tarehe 1 Septemba 1997 akateuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Angola.

Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili kunako tarehe 28 Juni 2001 akamhamishia nchini Chile hadi tarehe 29 Oktoba 2007, Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, alipomwmishia nchini Colombia. Hadi kuteuliwa kwake kuwa Balozi Mpya wa Vatican nchini Malta alikuwa Colombia.







All the contents on this site are copyrighted ©.