2013-02-13 10:20:33

Rais Obama anamshukuru na kumwombea Baba Mtakatifu Benedikto XVI


Baada ya Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita kutamka kwamba, anang'atuka kutoka madarakani hapo tarehe 28 Februari 2013, Rais Barack Obama, kwa niaba ya wananchi wa Marekani pamoja na Familia yake amempongeza Baba Mtakatifu kwa kusema kwamba, anamsindikiza kwa njia ya sala.

Rais Obama anaikumbuka ile siku walipokutana na Baba Mtakatifu mjini Vatican kunako mwaka 2009. Katika kipindi cha miaka minne, ameridhika na ushirikiano ambao wameoneshana katika miaka hii.

Rais Obama anasema kwamba, Kanisa linatoa mchango mkubwa nchini Marekani na katika Ulimwengu kwa ujumla. Anamtakia kila la kheri Baba Mtakatifu pamoja na kuwaombea Makardinali watakaokusanyika kwa ajili ya kumchagua Papa mwingine.







All the contents on this site are copyrighted ©.