2013-02-13 06:49:51

Huduma za Benki kwa njia ya mtandao zaanza kufanya kazi tena mjini Vatican


Huduma za Kibenki kwa njia ya mtandao zilizokuwa zimesitishwa hivi karibuni mjini Vatican kwa sasa zimerudishwa na kwamba, mahujaji, watalii na watumiaji wa huduma za Kibenki mjini Vatican wataweza tena kupata huduma hizi bila shida. Kwa sasa huduma za kibenki kwa njia ya mtandao zinaratibiwa na Shirika la Aduno kutoka Uswiss.

Hayo yamebainishwa na Padre Federico Lombardi, msemaji mkuu wa Vatican wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa Habari siku ya Jumanne, tarehe 12 Februari 2013. Amefafanua kwamba, watumiaji wa huduma za Benki kwa njia ya mtandao wataweza pia kulipia kwa njia ya Kadi za Benki wakati watakapokuwa wanatembelea Makumbusho ya Vatican. Shirika la Aduno linasemekana kuwa na uzoefu mkubwa katika shughuli za Kibenki Barani Ulaya.








All the contents on this site are copyrighted ©.