2013-02-08 11:52:33

Ajali yaua 53 Zambia na wengine 22 kujeruhiwa vibaya


Rais Michael Sata wa Zambia ametuma salam za rambi rambi kwa ndugu, jamaa na marafiki wa watu zaidi ya 53 waliopoteza maisha kutokana na ajali iliyotokea mjini Lusaka, Bus la abiria lilipogongana na Lori la migizo, siku ya Alhamisi, tarehe 7 Februari 2013. Waziri wa habari wa Zambia Bwana Kennedy Sakeni katika taarifa yake kwa vyombo vya habari anasema kwamba, jumla ya watu 22 waliojeruhiwa vibaya wamelazwa katika Hospitali mjini Lusaka.

Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa sababu ya ajali hii ambayo inasemekana kuwa ni mbaya kuwahi kutoka nchini Zambia katika miaka ya hivi karibuni. Mwezi Aprili 2005, Lori lililokuwa limebeba wanafunzi lilipinduka Kaskazini mwa Zambia na kusababisha vifo vya wanafunzi 38 na wengine 50 kujeruhiwa vibaya.







All the contents on this site are copyrighted ©.