Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Familia, Askofu Mkuu Vincenzo Paglia, ameungana
na Maaskofu wa Uingereza kupinga kupitishwa kwa pendekezo la Waziri Mkuu Cameron,
linalotaka kuhalalisha ndoa za mashoga, licha ya upinzani mkubwa uliopo. Jumatano
Chama cha Conservatives cha Uingereza kilipitisha pendekezo hilo, na hivyo kutoa nafasi
kwa muswada huo, kusonga mbele katika hatua ya kutajwa bungeni mwezi May mwaka huu.
Askofu Mkuu Vincenzo Paglia, akizungumzia pendekezo hilo, amesema, kwanza kabisa
anaungana na Maaskofu wa Uingereza kupinga uhalalishaji wa ndoa za mashoga , kama
pia alivyo onyesha mshikamano wake na Maaskofu wa Ufaransa kupinga sheria hiyo, ambayo
pia inapigwa na watu watu wote wenye mapenzi mema wa kila dini wakiwemo Wayahudi,
Waislamu,na imani za kijadi. Askofu Mkuu Paglia, ameutaja msimamo wa Kanisa Katoliki
kwamba, u wazi, ndoa huundwa na watu wawili wa jinsia tofauti mwanamme na mwanamke
na si vinginevyo.