Kwa muda wa siku tatu, Baraza la Kipapa kwa ajili ya Utamaduni, linafanya Mkutano
wake wa mwaka ulioanza tarehe 6-9 Februri 2013, , katika Ukumbi Mkuu wa Chuo Kikuu
cha LUMSA, Mtaa wa Borgo Sant’Angeli namba 13 hapa Roma. Mkutano unafanyika chini
ya uongozi wa Mkuu wa Baraza hilo, Kardinali Ginafranco Ravasi. Maudhui ya mkutano
yanalenga zaidi katika umuhimu wa Kanisa kuwasikiliza vijana kujifunza lugha yao na
kuzingatia thamani yao katika upendeleo wa kukutana na Kristu. Na pia umuhimu wa
kutoa nafasi kwa vijana hata ndani ya utendaji wa kanisa. Na Kanisa kuingia katika
utamaduni mpya wa tarakimu. Na hivyo, baraza limefungua Mkutano wake na Tamasha la
Muziki wa Rock.
Alhamis hii, Papa alikutana na wajumbe wa Mkutano huo. Na
katika hotuba yake, ameonyesha kufurahia maudhui ya mkutano huu unaochambua na kulenga
kuelewa nia na lugha ya vijana na kuimarisha yaliyo mema , katika mitazamo tofauti
tofauti inayojitokeza katika utamaduni wa vijana. "