2013-02-05 09:40:56

Rais Barack Obama anashiriki katika mkutano wa "Kifungua kichwa cha Sala Kitaifa"


Rais wa Chama cha Uhamsho wa Roho Mtakatifu nchini Italia Bwana Salvatore Martines kuanzia tarehe 5 hadi tarehe 7 Februari 2013 yuko Washington, DC, Marekani, kushiriki katika majadiliano ya sala yanayomshirikisha Rais Barack Obama na viongozi wengine waandamizi kutoka Marekani. Mkutano huu unajulikana kama kifungua kichwa cha Sala Kitaifa au kwa lugha ya umombo wenyewe wanasema "National Prayer Breakfast".

Kuna jumla ya wageni waalikwa 2000 kutoka pande zote za dunia na wawakilishi 160, watakaokusanyika ili kujadili mada mbali mbali zinazoendelea kutikisa dunia katika mapambazuko ya Karne ya Ishirini na moja. Lengo ni kuendelea na mchakato wa maboresho ya ushirikiano wa kimataifa unaojitambulisha kwa namna ya pekee katika mshikamano, maendeleo na huduma za kijamii zinazomgusa mtu mzima: kiroho na kimwili.

Mkutano huu kwa sasa unaingia katika toleo la sitini na moja, umeendelea kuwa ni Jukwaa kwa ajili kujenga na kuimarisha utamaduni wa mshimamano na udugu mintarafu tunu msingi za Kiinjili, daima wakitafuta mafao ya wengi, haki na amani. Ni mkutano unaowashirikisha viongozi wa kidini, kisiasa na kiuchumi,







All the contents on this site are copyrighted ©.