Viongozi wa kidini nchini DRC wanaitaka Serikali kuunda Tume huru ya Uchaguzi, kama
sehemu ya mchakato wa utawala bora. Wito huu umetolewa Padre Donatien Shole, Katibu
mkuu msaidizi Baraza la Maaskofu Katoliki DRC, wakati wa majadiliano kuhusu marekebisho
ya sheria yanayopania maboresho ya Tume ya Uchaguzi nchini humo, ili kuwezesha uchaguzi
kuwa huru na wa haki.
Viongozi wa kidini wanamwomba Rais Joseph Kabila ambaye
ana mamlaka ya kuweza kusukuma wazo hili na hatimaye likafanyiwa kazi na Bunge, kwani
wananchi wa DRC wanataka Tume huru inayojitegemea na itakayokuwa ni kwa ajili ya masilahi
ya wengi badala mwelekeo wa sasa kuonekana kuwa ni kwa ajili ya Chama Tawala. Tume
ya uchaguzi nchini humo, ilitupiwa lawama kali wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika
kunako Mwaka 2011.
Muswada wa sheria uliopendekezwa hauna masilahi kwa wananchi
wa DRC wanasema viongozi hawa wa kidini.