Tunalielekea dimbwi kubwa la hatari- Kardinali Bagnasco
Kardinali Angelo Bagnasco wa Jimbo Kuu la Genova, ambaye pia ni Rais wa Baraza la
Maaskofu Katoliki Italia, akitoa maoni yake juu ya mchakato unaoendelea kupiga hatua,
katika kuruhusu sheria ya ndoa za jinsia moja huko Ufaransa, amesema unaielekeza
pia Italia katika dimbwi kubwa la hatari. Onyo hilo amelitoa baada ya Bunge la
kwanza la Ufaransa kupitisha rasimu ya sheria , katika mchakato huo unaotafuta kuhalalisha
ndoa za jinsia moja. Na pia amereja maoni ynayotolewa katika gazeti la Italia la
kila siku la “Avvenire”yanayo shinikiza watu kukubali ndoa hizo. Eugenio Bonanata
anaripoti kwamba, Pamoja na uhamasishaji mkubwauliofanyika mitaani, watu wasikubali
kuupokea muswada wa sheria ya ndoa ya mashoga, bado Bunge la Ufarasa, limepitisha
rasimu ya ndoa za jinsia moja, ikiwa hatua nyingine ya kusonga mbele . Kwa rasimu
hiyo, kupiga hatua mbele , Rais wa CEI, ameionya na kuihimiza Italia isifuate Ufarasa,
hasa wakati huu inapopambana na mwelekeo wa kuzama pia katika dimbwi kubwa la hatari
ya utomvu wa maadili , ambao matokeo yake ni mbaya sana. Hofu ya Kardinali Bagnasco
hasa inajali kwamba, kupitishwa kwa sheria hiyo, ni hatua mbele katika madai mengine
ya mashoga, kupanga watoto, kama ilivyo kwa wanadoa ya mwanamke na mwanamme. Kardinali
anasema onyo lake si tu kwa nchi za Ulaya,ambazo zinasahau utamaduni wake asilia uliosmikwa
katika misingi ya Kikristo, bali kwa watu wote wenye kujali maadili ya Kijamii na
kumcha Mungu. Kardinali anaamini, uhuru huu unaozidi kiasi unatafuta kuiondoa
dini katika upeo wa macho ya binadamu . Na hivyo ni kufuru kubwa dhidi ya Mungu na
ubinadamu." Kardinali amesema hayo wakati wakati akiuhutumbia Mkutano wa Chama
cha Vijana Katoliki cha Azione Catolica, katika kuadhimisha Siku ya Kitaifa ya Utetezi
wa Maisha Italia. Ameihimiza Italia kuzingatia kwamba, familia ya mwanamke na mwanaume
haianzishwi na Serikali bali sheria za serikali zinapaswa kutetea na kudumisha asili
yake ya kimaadili , kiroho na kitamaduni, kama chimbuko asilia la watu.