2013-02-04 13:16:19

Mama Clinton abwaga manyanga baada ya utumishi wa miaka minne!


Hillary Clinton aliyekuwa Katibu wa Nchi Marekani, ameng'atuka kutoka madarakani na nafasi yake inachukuliwa na John Kerry ambaye amepanga kufanya mkutano wa ngazi ya juu kuhusu hali tete inayoendelea nchini Syria, lakini hakufafanua zaidi.

Katika hotuba yake, Clinton ambaye amekuwa madarakani kwa kipindi cha miaka minne amekiri kwamba, kufanya kazi katika idara hii nyeti inayohusu uhusiano wa kimataifa imekuwa ni heshima kubwa sana kwake. Lakini, Jumuiya ya Kimataifa inaishi katika wakati mgumu kutokana na kushamiri kwa vitendo vya kigaidi, vinavyotishia amani na usalama wa watu, kama ilivyojitokeza hivi karibuni kwa shambulizi dhidi ya Ubalozi wa Marekani Ankara, nchini Uturuki.







All the contents on this site are copyrighted ©.