Jumatatu hii umeanza Mkutano wa Kamati ya pamoja ya Makanisa ya Ulaya (CEC) mjini
Warszawa, katika Kituo cha Caritas cha Poland, ambako wajumbe kutoka makanisa 120
zikiwemo jumuiya za Kiotodosi , na Kipotestanti, na Halmashauri ya Baraza la Mabaraza
Katoliki ya Ulaya (CCEE) wameungana pamoja. . Mada kuu ya Mkutano ni "Imani
na dini katika Ulaya inayobadilika. Jumuiya mpya za Kikristo barani Ulaya ni changamoto
au nafasi . Mkutano huu unatajwa kuwa ni fursa kwa makanisa kutazama hali
halisi na kutafakari kwa pamoja , juu ya mabadiliko yanayofanyika katika uhusiano
mtu wa Ulaya na Mungu, na uzoefu wake wa kidini, na hasa ongezeko la jumuiya za Kiinjili
za Kipentekoste Ulaya. Kwa kuzingatia upana wa Mada , mkutano utazamishwa zaidi
katika kutazama uhusiano hadi matatizo ya kihistoria kwa makanisa na vikundi vipya
vya kikanisa , katika uwepo wake barani Ulaya, katika mtazamo wa kama ni changamoto
mpya au ni nafasi mpya za Uinjilishaji. Mandhari ya mkutano itaendelea kutegenezwa
na michango itakayotolewa na watalaamu, zaidi ya yote, matazamio ya kijamii na kihistoria,
kwa msaada wa Profesa Eileen Barker wa Shule ya Uchumi London. Watalaam wengine ni
Profesa Stanisław Wargacki wa Chuo Kikuu Katoliki cha Lublin; Na Kardinali Angelo
Bagnasco, Askofu Mkuu wa Genoa na pia Makamu wa Rais CCEE, pamoja na Askofu Mkuu
Metropolitan Yusufu wa Patriarki wa Kanisa la Kiotodox la Romania, ambao watalenga
zaidi katika uzoefu wa makanisa ya jadi yalivyo weza kudumu hadi mfumko wa makundi
mapya ya kikanisa. Pia Mstaafu Askofu Mkuu wa Southwark, Kevin McDonald, na Claire
Sixt-Gateuille mchungaji wa Kanisa la Reformed la Ufaransa, watalenga zaidi katika
kufafanua changamoto za kichungaji. Katika mkutano huo, washiriki watapewa taarifa
za mahusiano ya Wakristu na uekumene katiak uzoefu wa Poland, kama ilivyoandaliwa
na Askofu Krzyszrof Nitkiewicz, na Askofu Mkuu Jeremiasz, rais wa Baraza la Makanisa
nchini Poland. umatano Februari 6, mkutano utakamilika kwa wajumbe kufanya ziara
katika jengo la Makumbusho Maasi, wakitangulwia na kauli mbili: "Mwaka wa Imani, maadhimisho
ya miaka 50 ya Pili wa Vatican Baraza na Sinodi kwa Uinjilishaji Mpya" Wajibu wa
CEC katika Ulaya inayobadilika , Matazamio mapya, Maono na Misioni ".