2013-02-02 11:07:34

Zaidi ya watu 33 wateketea kwa moto mjini Mexico


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, amemtumia salam za rambi rambi Kardinali Norbert Rivera Carrera wa jimbo kuu la Mexico kutokana na moto mkubwa uliotokea kwenye Jengo la Makao Makuu ya Kampuni ya Mafuta Pemex inayomilikiwa na Serikali ya Mexico kati kati ya mji na hivyo kusababisha zaidi ya watu 33 kupoteza maisha yao na wengine zaidi ya 121 kujeruhiwa vibaya, mapema siku ya Ijumaa, tarehe 1 Februari 2013.

Ujumbe wa Baba Mtakatifu umeandikwa kwa niaba yake na Kardinali Tarcisio Bertone, Katibu mkuu wa Vatican, akionesha ukaribu wake kwa njia ya sala kwa wote waliofikwa na msiba huu. Ni matumaini ya Baba Mtakatifu kwamba, wahanga waliosalimika wataweza kupata msaada wa hali na mali kutoka kwa Wasamaria wema. Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, anawaweka marehemu wote chini ya ulinzi na maombezi ya Bikira Maria wa Guadalupe.







All the contents on this site are copyrighted ©.