2013-02-02 11:26:18

Mafuriko yanaendelea kuleta maafa nchini Msumbiji


Askofu Dionis Salomao Sengulane wa Jimbo la Lebombo, Kanisa Anglikani, Msumbiji anawaalika Wasamaria wema popote pale walipo kujitokeza ili kuwasaidia wananchi wa Msumbiji ambao wamekumbwa na mafuriko na watu zaidi ya mia moja, tayari wamekwisha kupoteza maisha na wengine laki moja na nusu hawana mahali pa kuishi baada ya makazi yao kukumbwa na mafuriko.

Kuna wanavijiji wengi ambao wamezunguka na maji kiasi kwamba, wanahitaji msaada wa dharura ingawa Serikali, Kanisa na Mashirika ya Misaada yanaendelea kutoa msaada, lakini hali bado ni mbaya sana anasema Askofu Sengulane. Kutokana na mafuriko, Serikali ya Msumbiji inahofia kwamba, pengine yakazuka magonjwa ya milipuko na hivyo kupelekea watu wengi zaidi kupoteza maisha yao.

Wananchi wa Msumbiji wanahimizwa kutunza usafi na kanuni za afya bora. Mafuriko haya yanaweza kusababisha wasi wasi mkubwa katika uhakika wa usalama wa chakula nchini humo kwa siku za usoni.







All the contents on this site are copyrighted ©.