2013-02-02 14:22:05

Askofu mkuu Michael A. Blume ateuliwa kuwa Balozi Mpya wa Vatican nchini Uganda


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, amemteua Askofu mkuu Michael August Blume kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Uganda. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Blume alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Benin na Togo, Barani Afrika. Itakumbukwa kwamba, alizaliwa kunako tarehe 30 mei 1946. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapewa Daraja Takatifu la Upadre hapo tarehe 23 Desemba 1972.

Akateuliwa na Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, kuwa Askofu mkuu hapo tarehe 24 agosti 2005 na kuwekwa wakfu hapo tarehe 30 Septemba 2005. Tangu wakati huo amekuwa ni Balozi wa Vatican nchini Benin na Togo.







All the contents on this site are copyrighted ©.