2013-02-01 11:16:48

Wafungwa 58 wafariki dunia nchini Venezuela kwa kushambuliana


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, ametuma salam za rambi rambi kwa Askofu mkuu Antonio Josè Lopez Castillo wa Jimbo kuu la Barquisimeto, Venezuela, kutokana na vifo vya watu 58 vilivyotokea hivi karibuni kwenye jela ya Uribana nchini humo, wakati wafungwa waliposhambuliana na Askari Magereza pamoja na kupelekea wafungwa wengine 90 kujeruhiwa vibaya.

Baba Mtakatifu katika ujumbe huu ambao umeandikwa kwa niaba yake na Kardinali Tarcisio Bertone, Katibu mkuu wa Vatican, anawasihi viongozi na taasisi mbali mbali nchini Venezuela, kuendelea kushirikiana katika mchakato wa kuleta maboresho ya maisha kwa wafungwa magerezani na kwamba, matukio kama haya yanayopelekea watu kupoteza maisha yao, hajajirudii tena kwa siku za usoni.







All the contents on this site are copyrighted ©.