2013-01-31 10:39:05

Muswada wa sheria ya ndoa za watu wa jinsia moja nchini Uingereza una madhara makubwa kwa wananchi!


Baraza la Maaskofu Katoliki Uingereza limewaandikia barua ya wazi Wabunge wa Uingereza kuonesha msimamo wao unaopinga muswada wa sheria unaotaka kuhalalisha ndoa za watu wa jinsia moja, kwani ndoa ni jambo nyeti sana linalogusa maisha ya watu wengi. Muswada wa sheria utakuwa na madhara makubwa katika historia na maisha ya wananchi wa Uingereza kwani ndoa inagusa uhusiano wa dhati kati ya bwana na bibi na matunda yake ni watoto wanaopaswa kulelewa: kiroho na kimwili.

Ni kwa njia ya watoto peke yake, kwamba, tendo la kujamiiana lina maana kubwa katika maisha ya Kijamii na hivyo linapaswa kuheshimiwa na kulindwa kisheria. Muswada wa sheria unaotaka kupelekwa Bungeni unafuta maana ya ndoa katika asili yake. Jambo hili ni nyeti lilipaswa kwanza kabisa kabla ya kujadiliwa na Wabunge, lipigiwe kura ya maoni.

Muswada huu wa sheria usifanyiwe mzaha kwani kuna madhara makubwa ambayo pengine Wabunge hawajayaona kwa sasa, mintarafu sheria binafsi, uhuru wa mtu kujieleza, uhuru wa kidini na elimu na kwamba, kunaweza kutokea misigano isiyo ya lazima kati ya Serikali na Kanisa.

All the contents on this site are copyrighted ©.