2013-01-31 15:16:32

Mh. Padre laurent Birfuorè Dabire ateuliwa kuwa Askofu Mpya wa Jimbo Katoliki la Dori, Burkina Faso


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, amemteua Mheshimiwa Sana Padre Laurent Birfuorè Dabirè, kuwa Askofu Mpya wa Jimbo Katoliki la Dori, Burkina Faso. Askofu mteule alizaliwa kunako tarehe 17 Septemba 1965 huko Dissin, Jimbo Katoliki la Diebougou, Burkina Faso. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kipadre katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana, kunako tarehe 29 Desemba 1995 akapewa Daraja Takatifu la Upadre.

Kama Padre amewahi kuwa Jaalim wa Seminari ndogo ya Saint Tarcisius, Jimbo Katoliki Diebougou. Kati ya Mwaka 1998 hadi Mwaka 2005 alipelekwa tena Roma kuendelea na masomo ya juu na hatimaye akajipatia shada ya uzamivu katika Sheria za Kanisa na zile za Kiraia. Kati ya Mwaka 2006 hadi mwaka 2008 alikuwa ni Jaalim wa Sheria, Seminari kuu ya Saint Jean Baptiste. Kuanzia mwaka 2011 hadi uteuzi wake, alikuwa ni Jaalim wa Sheria za Kanisa Chuo Kikuu cha "Unitè Universitarie de Bamako" nchini Mali.

Jimbo Katoliki la Dori lilikuwa wazi tangu tarehe 4 Novemba 2011 kufuatia hatua ya Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, kumhamisha Askofu Joachim Ouedraogo toka Jimbo Katoliki la Dori, kwenda Jimbo Katoliki la Koudougou, nchini Mali.All the contents on this site are copyrighted ©.