2013-01-31 15:15:41

Mh. Padre James Dembele ateuliwa kuwa Askofu Mpya wa Jimbo Katoliki la Kayes, Mali


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, amemteua Mheshimiwa Sana Padre Jonas Dembele kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Kayes, Mali. Askofu mteule alizaliwa kunako tarehe 15 Mei 1963 huko Sokoura, Jimboni San. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kipadre, akapewa daraja Takatifu la Upadre hapo tarehe 12 Julai 1992.

Tangu wakati huo amefanya shughuli mbali mbali za kitume kama Paroko Msaidizi, Paroko na Katibu wa Umoja wa Mapadre Wazalendo nchini Mali. Kunako mwaka 2008 hadi mwaka 2010 alitumwa na Askofu wake kujiendeleza kwa masomo ya juu kwenye Chuo Kikuu cha "Lumen Viate", mjini Brussels, Ubelgiji. Aliporudi kutoka masomoni alipewa dhamana ya kuanzisha Parokia Mpya ya Yasso, hapo mwaka 2011. Jimbo Katoliki la Kayes, Mali, lilikuwa wazi kutokana na kufariki dunia kwa Askofu Joseph Dao, kunako mwaka 2011.All the contents on this site are copyrighted ©.