Viongozi wa Israeli na Vatican wakutana mjini Yerusalemu
Tume ya kudumu ya pamoja kati ya Israeli na Vatican, tarehe 29 Januari 2013 imemaliza
mkutano wake wa pamoja. Monsinyo Ettore Balestrero, Katibu mwambata wa mambo ya nje
na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican ndiye aliyeongoza ujumbe wa Vatican na kwa
upande wa Israeli, alikuwa ni Bwana Daniel Ayalon, Waziri mdogo wa nchi za nje wa
Serikali ya Israeli.
Ujumbe wa Vatican umetoa pongezi za dhati kwa wenzao
wa Israeli kwa majadiliano ambayo yanalenga kujenga na kudumisha mafao ya pande hizi
mbili. Kwa pamoja wamechambua mafanikio yaliyokwisha kupatikana hadi sasa na wanatazamia
kwamba, Makubaliano haya yataweza kufikiwa muafaka mapema iwezekanavyo. Tume hii itakutana
tena mwezi Juni 2013 hapa mjini Vatican.