Maaskofu wa Kanisa la Babiloni la Caldea laanza Maadhimisho ya Sinodi kumchagua Patriaki
Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, ameitisha Sinodi ya Maaskofu wa Kanisa la
Babiloni ya Caldea, itakayokuwa chini ya uongozi wa Kardinali Leonardo Sandri, Rais
wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki. Pamoja na mambo mengine Sinodi
hii itakuwa na dhamana ya kumchagua Patriaki wa Kanisa la Babiloni ya Caldea.
Jumatatu,
tarehe 28 Januari, 2013 wameanza Sinodi hii kwa mafungo ya kiroho, wakimwomba Roho
Mtakatifu ili aweze kuwasaidia katika maadhimisho ya tukio hili ambalo kimsingi linajisimika
katika sala, tafakari pamoja na kumegeana uzoefu na mang'amuzi katika maisha na utume
wa Kanisa.