2013-01-29 07:39:04

Kumbu kumbu ya miaka 100 ya Padre Werebrief Van Straaten, Mwanzilishi wa Shirika la Msaada kwa Makanisa hitaji


Shirika la Kipapa kwa ajili ya Makanisa hitaji hapo tarehe 31 Januari 2013, litaadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kumkumbuka Hayati Padre Werenfried Van Straaten, siku ambayo aliitupa mkono dunia, yapata Karne moja iliyopita.

Maadhimisho ya Mwaka huu ni muhimu sana kutokana na ukweli kwamba, Mama Kanisa anamshukuru Hayati Padre Werenfried kutokana na ujasiri wake uliosaidia kuanzisha Shirika hili ambalo limekuwa ni msaada mkubwa kwa wanafunzi kutoka katika nchi za kimissionari wanaosoma na kuishi hapa mjini Roma; limeendelea kutoa msaada wa hali na mali kwa Makanisa yanayodhulumiwa sehemu mbali mbali za dunia.

Ibada ya Misa takatifu itaadhimishwa kwenye Kanisa kuu la Bikira Maria Trastevere. Kutakuwepo na wawakilishi kutoka Bielorussia, Cuba, Nigeria na Pakistan na itaongozwa na Monsinyo Sante Babolin, Rais wa Shirika la Kipapa kwa ajili ya Makanisa hitaji, nchini Italia.
All the contents on this site are copyrighted ©.