2013-01-28 09:38:17

Mshikamano wa Chama cha Vijana wa Italia kwa Watoto wanaoishi katika mazingira magumu Alexandria, Misri


Zaidi ya Vijana Wakatoliki elfu mbili kutoka Parokia mbali mbali za Jimbo kuu la Roma wakiwa pamoja na Wazazi, Walezi na Mapadre wao, Jumapili iliyopita, tarehe 27 Januari 2013 walifanya Maandamano ya Amani hadi kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, kama hitimisho la Mwezi wa Amani, ambao unawachangamotisha watoto hawa kuwa wadau katika ujenzi wa misingi ya amani katika maeneo wanamoishi.

Vijana wawili ambao waliwawakilisha wenzaobaada ya kusoma risala yao kwa Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, walirusha njiwa wawili kama alama ya kuombea amani sehemu mbali mbali za dunia. Mwenyezi Mungu anamtakia amani kila mtu, bila kujali uwezo, hali pamoja na makando kando ya maisha.

Vijana hawa pia wamewasilisha mchango wao kutoka na sadaka waliyoifanya kwa kipindi chote cha Mwezi Januari pamoja na mchango wa Parokia zao kwa ajili ya kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu nchini Msiri, mradi unaosimamiwa na na Wayesuiti mjini Alexandria.

Maandamano ya Umoja wa Vijana Wakatoliki Italia kwa mwaka huu yameongozwa na kauli mbiu "tuone kama unaweza"! Wamemhakikishia Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita kwamba, wanampenda na kumwombea. Hata katika ujana wao, wanapenda kuwa ni wadau wa ujenzi wa amani, kwa kujenga utamaduni wa kuheshimiana. kuthaminiana na kutoa haki kwa wote.All the contents on this site are copyrighted ©.