2013-01-28 10:00:41

Jumapili ni Siku ya Bwana!


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, Jumapili iliyopita, tarehe 27 Januari 2013, ujumbe wake katika Twitter anauliza swali la msingi, Jumapili kwetu ina maana gani? Ni Siku ya Mapumziko na Familia, lakini kwanza kabisa ni Siku ya Bwana.

Itakumbukwa kwamba, Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili, katika Waraka wake wa Kichungaji, Dies Domini, Siku ya Bwana anasema kwa ufupi kwamba, hii ni Siku ya Mungu kwani aliweza kupumzika baada ya kazi ya uumbaji! Ni Siku ya Kristo, kwani Kanisa lifanya kumbukumbu ya Fumbo la Pasaka, yaani: mateso, kifo na ufufuko wa Kristo.

Ni Siku ya Kanisa, inayowaungaanisha waamini kutoka katika: Familia, Jumuiya, Vigango na Parokia zao kushiriki katika Liturujia ya Neno la Mungu pamoja na Liturujia ya Ekaristi Takatifu; changamoto kwa waamini kuwa ni Eukaristia kwa jirani zao.

Ni Siku ya Mwanadamu, kwani hapo anapaswa kupumzika ili kujichotea nguvu za kuweza kukabiliana na majukumu yake ya kila siku, bila kusahau kufanya matendo ya huruma, kama njia ya kuitakatifuza Siku ya Bwana. Mwishoni, Siku ya Bwana ni fursa ya kutafakari mambo ya nyakati kwa kutambua kwamba, hapa duniani, mwanadamu ni mpita njia tu.

Ndugu msikilizaji wa Radio Vatican, unaweza kujichotea utajiri wa ujumbe huu mfupi katika lugha zifuatazo: Kilatini, Kiitalia, Kiingereza, Kifaransa, Kireno, Kihispania, Kijerumani, Kipolandi na Kiarabu.

Dominica tandem dies quid nobis importat? Propria quidem domi focique est dies. Atqui pertinet in primis ad Ipsum.


Che cosa significa per noi la Domenica, giorno del Signore? E’ un giorno per il riposo e la famiglia, ma prima di tutto un giorno per LuiWhat does Sunday, the day of the Lord, mean for us? It is a day for rest and for family, but first of all a day for Him.
Que signifie pour nous le dimanche, jour du Seigneur? C’est un jour pour la famille et le repos, mais c’est d’abord un jour pour le SeigneurQual é o significado do domingo, dia do Senhor, para nós? É um dia para o descanso e para a família, mas em primeiro lugar é um dia para Deus.
All the contents on this site are copyrighted ©.