2013-01-28 11:02:39

Bajeti kwa Ofisi ya Rais, Majeshi, Ulinzi na Usalama nchini Angola bado ni kubwa mno!


Taarifa kutoka nchini Angola zinabainisha kwamba, Bunge la Angola limepitisha bajeti ya kiasi cha kwanza trillioni 6.6, sawa na kiasi cha dolla za Kimarekani billioni 69, sawa na ongezeko la asilimia 50% za Bajeti ya Serikali, ikilinganishwa na mwaka 2012.

Kiasi cha asilimi 33.5% ya bajeti nzima kitatumika katika sekta ya: afya, elimu, miundo mbinu, ujenzi wa makazi kwa wananchi maskini nchini Angola, utunzaji wa mazingira pamoja na huduma za kijamii.

Wachunguzi wa bajeti nchini Angola wanasema kwamba, kiasi cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya matumizi ya Ofisi ya Rais, Majeshi, Ulinzi na Usalama bado ni kiwango cha juu kabisa, ikilinganishwa na fedha ya bajeti iliyotengwa kwa maendeleo ya jamii na huduma kwa raia.All the contents on this site are copyrighted ©.