Tahariri ya Padre Federico Lombardi kwa wiki hii , imetazama kwa makini Wiki la Kuombea
Umoja wa Wakistu, kuwa ni nafasi ya maombi kwa ajili ya umoja wa Wakristu, unaoonyesha
utendaji wa hali ya juu wa onyesha moyo wa kiekumeni. Ni tendo linalotoa maana
na kulisha mipango mingine yote katika juhudi zilizoanzishwa za Kiekumeni ambazo
katika umuhimu wa tabia yake ya tamaduni au mazungumzano ya kiteolojia na hisani
zingine za kijamii, na kadhalika, yote yanakuwa ni mema na muhimu. Lakini hasa
inatakiwa kuchota kutoka ndani roho wa umoja wenye kuwahamasisha wote, kuungana
ktiak majitolea ya sala ya moja kwa moja na sala kuu kwa Yesu, kwa ajili ya umoja
wa wale wanao mwamini Yeye.