2013-01-26 15:53:17

Papa aongoza Ibada ya kufunga Wiki la Sala ya Kiekumene ...


Baba Mtakatifu Benedikto XVI, Ijumaa aliongoza Ibada ya Kiekumene ya Masifu ya jioni , katika Kanisa Kuu la Mtakaifu Paulo nje ya kuta Roma, kwa nia ya kufunga wiki la sala ya kuomba Umoja wa Wakristu.
Nia ya sala katika wiki hili, ni kujenga umoja, mshikamano na ushirikiano wakuonekana wa Wakristu, katika dunia ya leo, kama mashahidi wa Bwana mmoja Yesu Kristu, kama yeye mwenyewe alivyosali, kwa Baba yake, Baba ulionipa na wawe wamoja kama sisi tulivyo wamoja.
Wiki la sala ni juhudi zilizoanzishwa na Padre Mkatoliki Paulo Wattson kunako mwaka 1908.
Baba Mtakatifu katika homilia yake alionyesha kujali jinsi jamii ya sasa inavyolazimika kupambana na vitisho vya mambo ya kidunia, na hivyo kuwa changamoto kwa makanisa yote na ujumuiya za Kikanisa, kukabiliana na hali hiyo.
Na kwamba umoja wenyewe ni nafasi ya kipekee katika ufanikisha uinjlishaji thabiti kwa wote waliokwisha lisikia neno na wale ambao bado kabisa kuisikia habari njema ya Injili, nguvu ya uponyaji na wokovu.
Papa aliendelea kusema, Kashfa ya utengano na migawanyiko inayodharirisha kazi za kitume ilikuwa ni msukumo ulioanzisha juhudi hizi za kiekumene , tunazozijua leo hii. Na muungano kamili wa kuonekana kati ya Wakristu unaweza kueleweka, katika kweli kwamba ni, kama tabia ya ushuhuda wazi wa Mkristu.
Papa alitoa wito kwa wakristu wote, kutembea katika njia ya kuelekea umoja kamil, kuwa jambo muhimu kwa Wafuasi wote wa Kristu, na si maneno tu lakini ionekane kwa vitendo, ushirikiano wa karibu zaidi katika njia hii ya imani katika dunia ya nyakati hizi. Leo hii, kuna haja kubwa zaidi ya kuonyesha maridhiano na maelewano tena kwa uthabiti na uwazi zaidi katika kama utamaduni halisi wa Wakristu wa leo hii.








All the contents on this site are copyrighted ©.