Nchi za Amerika ya Kati, S.I.C.A zinathamini mchango wa Vatican katika mchakato wa
maendeleo endelevu!
Askofu mkuu Luigi Pezzuto, Balozi wa Vatican nchini El Salvador pamoja na Dr. Juan
Daniel Aleman Gurdian, katibu mkuu wa Mfumo wa Maendeleo Amerika ya Kati, S.I.C.A,
wametiliana sahihi Mkataba unaoifanya Vatican kuwa ni nchi mwanachama mtazamaji kutoka
nje ya Amerika ya Kati.
Tukio hili limehudhuriwa na mabalozi pamoja na wawakilishi
wa nchi za Amerika ya Kati, hapo tarehe 21 januari 2013. Huu ni utekelezaji wa maamuzi
yaliyotolewa na Wakuu wa Serikali wanachama wa S.I.C.A kwa kuruhusu Vatican kuwa nchi
mwanachama kutokana na mchango wake katika mchakato wa kumletea mwanadamu maendeleo
endelevu: kiroho na kimwili; dhamana inayotekelezwa na Makanisa mahalia katika sekta
ya elimu, afya, jamii, utamaduni, haki, amani na usalama wa kidemokrasia.