2013-01-26 16:01:30

Mahakama ya Kitume ya Rota Romana yazindua kipindi kipya cha mwaka wa Kazi


Mamlaka ya Mahakama ya Kitume ya Kanisa Katoliki , yanayojuliakna kwa jina Rota Romana, Jumamosi yalizindua kazi za mwaka huu, kwa Ibada ya Misa ya Ekaristi iliyo ongozwa na Karidnali Tarcisio Bertone , katika Kikanisa cha Paolina.
Kardinali Tarcisio, katika homilia yake, aliwataka wajumbe wa Mahakama ya Rota Romana, kuwa kama walivyokuwa watanguzi wao, kutazama sana maonyo ya Mtakatifu Paulo na kuwa na ujasiri wa kutenda kwa haki na ukweli wa Kanisa, bila ya kuonea haya, shuhuda za Kanisa la Kristu na kuwa wavumilivu wa kutegemea "nguvu ya Mungu kama ilivyoandikwa katika waraka wa Mtume Paulo kwa Timoteo " (2 Tim 1:08),

Na kwamba katika dunia ya nyakati hizi, ambayo kwa bahati mbaya imemezwa na vita, familia kuvurugwa na chuki na uadui, wengi wakiwa wamechoka na kukosa imani, kila mtu sasa anaitwa na Kanisa kutangaza amani na haki ya Mungu katika Kristo Yesu. Na ni kufikisha popote huduma na kazi za kitume za Kanisa zinazo onyesha ishara ya Ufalme wa Mungu, kwa wale wanaompokea Kristu. Ni huduma ya kutoa kila kitu bure na kuwapa wote kwa bure: upendo na huruma ya Kristu. K
Kardinali alieleza na kuweka bayana kwamba, wao si mabwana wa Neno wanalo lihubiri, wala watu wanaowahubiria. Lakini wao ni watumishi wa mmoja kwa mwingine , wakizifanya kazi kwa nia na neema ya Mungu kwa ajii ya wote, kwa ajili ya kuokoa kila mmoja kwa gharama ya mwingine.
Ni Kuishi na utambuzi huu kama matokeo ya tabia ya utendaji wa kila siku, ikimaanisha , kutengeneza nafasi kwa ajili ya uwepo wa utendaji unaoongozwa na Roho Mtakatifu, aktiak utendaji wa haki na ukweli.
Kardinali alimaliza kwa kuomba Msaada wa Mama Mtakatifu Sana Bikira Maria, Mama wa Kanisa, Bibi arusi wa Roho Mtakatifu na kupitia nguvu ya maombezi yake, dhabihu walizotolea katika Ibada, ziweza kuwapa zawadi ya hekima na akili, ili daima wapokee na kufanywa upya mantiki ya kweli wa Injili, kigezo pekee katika utoaji wa hukumu za kweli na huruma.
All the contents on this site are copyrighted ©.