2013-01-25 15:07:35

Barua mbili binafsi za Papa kuhusu seminari na Katekesi zimechapishwa rasmi.


Ijumaa hii, kumechapishwa barua mbili binafsi za Kitume za Baba Mtakatifu Benedkto XV1( Motu Proprio), ambazo zinahamisha mamlaka ya seminari kutoka Shirika kwa ajili ya Elimu Katoliki, na kuingia katika shirika kwa ajili ya Mapadre. Na mamlaka yanayosimamia Katekesi kutoka katika shirika la Makreli, na kuingia katika Shirika la Kipapa kwa ajili ya Ukuzaji wa Uinjilishaji Mpya .
Barua hizo mbili zilitangazwa na Papa Oktoba 27, 2009, wakati wa kukamilika kwa Sinodi juu ya Uinjilishaji mpya.
Wakati wa kutangaza nia hizo mbili Papa alisema, "Katika mazingira ya tafakari za Sinodi ya Maaskofu," Uinjilishaji Mpya kwa uenezaji wa Imani ya Kikristo, "na katika kufunga mchakato wa kutafakari juu ya mandhari ya semina na Katekesi, na baada ya kutolea sala na tafakari za kina zaidi , nimeamua kutangaza kwamba, kuna haja ya kufanya mabadiliko ya kuhamisha mamlaka yanayosimamia Seminari kutoka Shirika la Elimu Katoliki, yahamie katika Shirika la Makreli. Na pia Mamlaka yanayosimamia Katekesi, ihame kutoka shirika la Mapadre na kuingia katika Baraza la Kipapa kwa ajili ya Kukuza Uinjilishaji Mpya .
Barua hizo mbili zilizoandikwa na Papa katika lugha ya Kilatini, zimetathmini umuhimu wa malezi ya kipadre katika umuhimu wake kama Makuhani wa Bwana. Kwa mtazamo huo, barua ya kitume ya Papa , inatoa dhamana kwa Shirika la Mapadre ,kusimamia kazi zote zinazohusiana mafunzo, maisha na huduma za kichungaji katika miito ya Mashemasi na Mapadre na uteuzi wa wale wanaowania kujiunga na Madaraja Matakatifu, yakiwemo pia masomo yao ya kawaida na ya kiroho , mafundisho ya Kanisa na kazi za kichungaji seminarini na katika vituo vingine kwa ajili ya mashemasi wa kudumu, na katika kuiendeleza elimu yao, pamoja na hali ya halisi za maisha na taratibu kwa ajili ya huduma na usalama wao katika jamii. "

Kwa barua mpya juu ya seminari, Shirika la Elimu Katoliki, lililokuwa likishughulika na seminari na Taasisi za Elimu kwa sasa linapata jina jipya " Mamlaka ya Elimu ya Falsafa na Tauhidi , kama ilivyoshauriwa na Shirika la Mapadre.

All the contents on this site are copyrighted ©.