2013-01-24 14:56:45

Uwasilishaji wa Ujumbe wa Papa kwa ajili ya adhimisho la 47 la Siku ya Mawasiliano Jamii.


Askofu Mkuu Claudio Maria Celli, amewasilisha Ujumbe wa Papa kwa ajili ya adhimisho la 47 la Siku ya Mawasiliano Duniani, itakayo adhimishwa tarehe 12 May 2013. Ujumbe wa Papa,unaongozwa na Kauli mbiu: Mifumo ya mawasiliano jamii Nafasi Mpya za Uinjilishaji.
Hotuba ya Askofu Mkuu Claudio Maria Celli, kwa ajili ya uwasilishaji huo, imepembua yaliyomo katika ujumbe wa Papa , ikiangalia pia , matokeo ya takwimu za tafiti zilizofanyika katika nchi za 21 za bara tano.
Askofu Mkuu Celli ametaja kati ya yaliyoainishwa katika takwimu hizo ni pamoja na madhara hasi ya matumizi ya mitandao ya habari katika maendeleo ya watu, kama ilivyoelezwa na Mwandishi mmoja wa vitabu wa Marekani, jinsi mfumo huu mpya wa internent unavyoweza kufanya mazuri mengi kwa kasi ,lakini wakati huohuo, pia unaonekana kupumbaza akili za watu , au kuwafanya kuwa wavivu wa kufikiri kwa kina. Na hivyo anaonyesha kushakia iwapo mtandao huo, hauna mwelekeo wa kupumbaza na kubadilisha akili za watu.
Kwa muktadha huu, Askofu Mkuu ameuangalia ujumbe huo wa Papa , akisema, ujumbe unaonyesha pia tathimini chanya za kijamii kwa vyombo vya habari, kwamba yote si mabaya, lakinii pia ni fursa kwa ajili ya mazungumzo na majadiliano, hasa katika utambuzi wa uwezo wake, katika kuimarisha mahusiano ya pamoja au miongoni mwa watu kwa ajili ya kukuza ufanisi wa maelewano ya familia ya binadamu.
Hata hivyo, kwa ajili ya kufanikisha hili, Ujumbe umeasa, ni muhimu kuheshimu faragha za watu na kuwajibika katika kutoa habari za kweli na uhalisi wa kushirikisha, si tu taarifa na tambuzi, lakini kama sehemu ya kiini cha mawasiliano kati ya watu.
Na pia umegusia mabadiliko ya mienendo ya kijamii katika vyombo vya habari, ukisisitiza umuhimu wa kuingizwa katika jitihada na hasa zaidi katika kuzingatia moyo wa ubinadamu, kwenye vipindi vya mwingiliano wa maswali na majibu,kwa ajili ya kutoa maana ya uwepo wa binadamu.

Kwa mtazamo huo, Askofu Mkuu Celli, ameutaja ujumbe wa Papa kwamba, unagusa maeneo mengi muhimu katika maisha ya kijamii, na hivyo kama ilivyosema kauli mbiu ya ujumbe huo, inakuwa ni nafasi nzuri ya uinjilishaji mpya , kazi ya kulitangaza Neno, Kama Yesu Kristu Mwenyewe alivyoagiza.
All the contents on this site are copyrighted ©.