2013-01-24 09:53:08

Maafa nchini Malawi! Watu 641 hawana makazi kutokana na mvua kubwa


Zaidi ya familia 641 kutoka Uwambo, Wilaya ya Zomba, Malawi hawana makazi baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko hivi karibuni kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyeesha nchini humo. Mvua hii pia imesababisha uharibifu mkubwa wa mazao mashambani baada ya mafuriko hayo kuharibu pia Bwawa lililokuwa limejengwa ili kudhibiti maji.

Waathirika hawa wanahitaji msaada wa dharura ili kuweza kukabiliana na hali hii ngumu. Kwa sasa watu wanahitaji: chakula, maji safi na salama, nguo na blanketi za kujifunika. Licha ya vifo vilivyotokea lakini pia kuwa watu 5,000 ambao wamepoteza kila kitu kutokana na mafuriko hayo. Serikali ya Malawi inaendelea kujikakamua kutoa msaada kwa waathirika hao.All the contents on this site are copyrighted ©.