2013-01-23 09:15:19

Waachieni Mapadre mliowateka, ili wamtumikie Mungu na Jirani zao!


Baraza la Maaskofu Katoliki DRC limerudia tena ujumbe wake, kwa kuwaomba watu ambao waliwateka nyara Mapadre watatu wa Shirika la Assumption, Mwezi Oktoba 2012 kuwaachia mara moja, ili waweze kuendeleza huduma kwa waamini wao kiroho na kimwili.

Maaskofu wanasema, Mapadre hawa waliotekwa hawana sababu ya kuendelea kuteseka katika mazingira hayo. Ni nafasi kwa wateka nyara kutubu na kuongoka, kwa kuwaachia ili waendelee kutekeleza wajibu wao. Mapadre waliotekwa tangu mwezi Oktoba, 2012 ni Jean Pierre Ndulani, Anselme Wasikundi pamoja na Padre Edmond Bamutate.

Mapadri hawa walitekwa nyara hapo tarehe 19 Oktoba 2012 walipokuwa kwenye Parokia ya Notre Dame des Pauvres iliyoko Mbau, Jimbo Katoliki la Butembo, DRC. Tangu wakati huo, hakuna taarifa juu ya Mapadre hawa.All the contents on this site are copyrighted ©.