2013-01-23 15:23:59

Papa ampokea Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha Vietnam


Mapema siku ya Jumanne, Baba Mtakatifu Bendikto XV1, alimpokea Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunist cha Vietnam , Mheshimiwa Nguyen Phu Trong, akiwa ameandamana na ujumbe wa watu kumi kutoka chama hicho , akiwemo pia Naibu Waziri Mkuu Nguyen Xuan Phuc. Tukio hili linatajwa kuwa la kipekee kutokana na kwamba, hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Papa kukutana na Katibu wa Chama cha Kikomunisti cha Vietnam.
Ujumbe huo baada ya kukutana na Papa , ulikutana pia na KatibuMkuu wa Vatican Kardinali Tarcisio Bertone . Na mazungumzano yao yaliyofanyika katika hali za kirafiki , yakilenga zaidi, hoja zinazovutia pande zote mbili, Vietnam na Vatican , hasa tumaini la kupata suluhu katika baadhi ya masuala ambayo bado yanatia uvuli, katika mahusiano wa nchi hizi mbili, hasa uimarishaji wa uhusiano na ushirikiano wa karibu zaidi.
Katibu Mkuu Nguyen Phu Trong tangu mwaka 2011, amekuwa akifanya ziara Vatican kama sehemu ya ziara zake za kutembelea Ulaya. Na kwamba , tangu kuanzishwa kwa mazungumzano mwaka 2007 kati ya Hanoi na Jimbo la Papa , hatua nzuri zimepigwa katika mahusiano ya nchi hizi . Novemba iliyopita, , Ujumbe kutoka Ofisi ya Mahusiano ya Kidini pia ilitembelea Vatican. Na Januari 2011, aliteuliwa Askofu Mkuu Leopoldo Girelli, asiye raia wa Vietnam, kuwa mwakilishi wa Vatican kwa Serikali ya Vietnam.
Jumatatu Katibu Mkuu Trong huyo alikutana na Rais Georgio Napolitano wa Italy na anatazamia kukamilisha ziara yake katiak nchi za Ulaya Magharidi, Alhamis kwa kutembelea London Uingereza.
Kwa mujibu wa takwimu Katoliki , Vietnam kuna wakatoliki wapatao millioni sita ambao ni katibia na asilimia saba ya raia wote wa Vietnam.








All the contents on this site are copyrighted ©.